News

SERIKALI YALIPA FIDIA YA SHILINGI MILIONI 999 KWA WANANCHI 103 WA DODOMA KWA MIRADI YA MAJI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Maji, imekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia yenye jumla ya Shilingi Milioni 999 kwa wananchi 103 ambao ardhi yao ilitwaliwa katika maeneo ya Nzuguni, Zuzu Nala, Nala Chihoni na Kibaigwa kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA). Read More
Posted On: Aug 13, 2025

DUWASA NA VEI WASAIDIA 'UNIFORM' ZA SHULE KWA SHULE SABA ZA MSINGI KIBAIGWA, KONGWA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kushirikiana na Dutch Water Operators (VEI) wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi 105 wa shule Saba za Msingi zilizopo Kata ya Kibaigwa, Wilayani Kongwa. Read More
Posted On: May 16, 2025

WADAU SEKTA YA MAJI MALAWI WATEMBELEA DUWASA
Februari 05, 2025, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imepokea ugeni kutoka Kampuni ya Usambazaji Maji ya Salima Lilongwe Water Supply Company (SLWSC) ya nchini Malawi kwa lengo la kujifunza namna DUWASA inavyoendesha shughuli zake za uzalishaji na usambazi maji. Read More
Posted On: Feb 06, 2025

MSIZOEE SHIDA ZA WANANCHI - AWESO AWAASA DUWASA
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb.), amewaasa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuacha kuzoea shida za wananchi, na badala yake kuzitafutia ufumbuzi ili wananchi wapate huduma ya Majisafi ya uhakika. Read More
Posted On: Jan 15, 2025

WAZIRI AWESO ANADI MIRADI YA MAJI KOREA
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb) ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya EXIM ya Korea ambayo imefadhili utekelezaji wa miradi ya Majitaka nchini Tanzania yenye jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 248.3 (Mkoa wa Dar es Salaam 90 $US milioni, Dodoma 70 $US million; na Iringa 88.3 $US million). Read More
Posted On: Dec 11, 2024

DUWASA YATANGAZA OFA KWA WATEJA WAKE
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Lena Mwakisale ametangaza ofa maalumu kwa wateja wake wote waliositishiwa huduma ya maji kulipia nusu ya deni na faini ili kuweza kurudishiwa huduma hiyo. Read More
Posted On: Dec 11, 2024