News

Posted On: Oct, 10 2025

​DUWASA - CHAMWINO YATAMBUA THAMANI YA MTEJA

News Images

Katika kuendeleza Wiki ya Huduma kwa Mteja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Kanda ya Chamwino wameendelea kutembelea na kutoa shukrani kwa wateja.

DUWASA - Chamwino Oktoba 08, 2025 imetoa Tuzo ya Shukrani kwa Mteja Mkubwa, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makao Makuu Chamwino, ambapo Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa Kambi Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino Dodoma, Kanali Geofrey Mvula.

Kanali Mvula ameishukuru na kuipongeza DUWASA kwa kutambua mchango wao na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi na kusisitiza kuendeleza uhusiano mzuri kati ya JKT na DUWASA.

Kwa upande wake Meneja wa DUWASA, Kanda ya Chamwino, Bw. Gray Mbalikia amesema Tuzo hiyo ni ya shukrani kwa JKT kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka.

Pia DUWASA imetoa msaada wa mahitaji na vifaa mbalimbali katika Shule Msingi ya Wasioona ya Buigiri, ikiwa ni sehemu ya kutambua makundi yenye uhitaji.

Wiki ya Huduma kwa Mteja 2025 ina Kauli Mbiu isemayo "Dhamira Inawezekana" ambayo imeanza Oktoba 06, 2025 na itahitimishwa ifikapo Oktoba 12, 2025.