News
DUWASA - BAHI YASHIRIKISHA WADAU WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Kanda ya Bahi Leo Oktoba 07, 2025 imezindua Wiki ya Huduma kwa Mteja ikilenga kuimarisha uhusiano na wateja wake.
Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi za DUWASA, Kanda ya Bahi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mdau Mkubwa wa DUWASA, Ndugu Maximilian Kafulya, Mfanyabiashara wa Mazao na Nafaka.
Akizungumza katika Uzinduzi huo wa Wiki ya Huduma kwa Mteja, Ndugu Kafulya ameishauri DUWASA kuendelelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Ninaipongeza DUWASA kwa kuendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi na tunatambua jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa majisafi na salama", amesema Ndugu Kafulya.
Wiki ya Huduma kwa Mteja inatarajiwa kuwapa fursa wananchi na wateja wa DUWASA kuzifahamu huduma zinazotolewa pamoja na kuwasikiliza wateja