News
Posted On:
Oct, 10 2025
DUWASA - KUBAIGWA MTAA KWA MTAA - WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyoanza Oktoba 06, 2025, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Kanda ya Kibaigwa wameendelea kutekeleza Kampeni ya Mtaa kwa Mtaa kwa kuwatembelea baadhi ya wateja ili kupata maoni, kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo za huduma ya maji.
Aidha, DUWASA - Kibaigwa imetoa tuzo ya shukrani kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibaigwa akiwa Mteja Mkubwa na mlipaji mzuri wa huduma.
Naye Meneja wa DUWASA - Kanda ya Kibaigwa, Bw. Salum Haji amesema Tuzo ya Shukrani iliyotolewa kwa shule hiyo ni kuonesha ushirikiano mzuri uliyopo kati ya Mamlaka na wateja wake.
Wiki ya Huduma kwa Mteja kwa mwaka 2025 ina Kauli Mbiu inayosema "Dhamira Inawezekana"