News

Posted On: Oct, 10 2025

DUWASA KANDA YA KONGWA YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi Mazingira Dodoma (DUWASA) Kanda ya Kongwa imezindua Wiki ya Huduma kwa Mteja kwa kushirikiana na wadau wake.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyofanyika Oktoba 07, 2025, Mgeni rasmi Mkuu wa Shule ya St. Francis, Ndugu Gadiel Kitomari, amesisitiza kuwa shule anayoiongoza inapata huduma ya majisafi ya uhakika ikizingatiwa kuna idadi kubwa ya wanafunzi.

“Tunajua umuhimu wa maji kwa wanafunzi wetu, na hasa kwa wanafunzi wasichana ambao wana hitaji kubwa la majisafi. Hii ndiyo sababu tunakuwa wateja wakubwa na walipaji wazuri. Tunasema asanteni kwa uwajibikaji wenu pale tunapohitaji msaada,” alisema Ndugu Kitomari.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Wilaya ya Kongwa, Bw. Rogert Iranga, ameipongeza DUWASA kwa ushirikiano wanaotoa.

“Tunafurahi sana kwa ushirikiano mwema na DUWASA. Tunawahakikishia kuwa tutaendelea kudumisha ushirikiano huu mzuri ili tuendelee kupata huduma bora kutoka kwenu aliongeza Bw. Iranga.

DUWASA imejipanga kutumia Wiki ya Huduma kwa Mteja, kutoa elimu juu ya huduma zinazotolewa na Mamlaka, kupokea malalamiko na kutatua kero zinazowakabili Wateja.

" Dhamira Inawezekana"