News
Posted On:
Jun, 17 2026
WAZIRI KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MAJI - WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametembelea Banda la Wizara ya Maji na Taasisi zake kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi Umma, 2026.
Katika Maonesho hayo yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma, Mhe. Kikwete amepata maelezo kuhusu Gridi ya Maji ya Taifa na baada ya kutembelea mabanda alifungua Rasmi Maonesho hayo yakiwa na Kauli Mbiu ya "Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi Kwa Huduma Endelevu"