UKOSEFU WA MAJI
Posted On: Jun 16, 2026
Ndugu Mteja na Mdau wetu, kutokana na taarifa hii ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya katizo la umeme kwenye visima vya maji vya Kilungule, Mamba ya Mbali na Kituo cha kusukuma maji cha Mzakwe tarehe 19 Juni 2026 ili kuruhusu kazi hiyo muhimu kufanyika, hali hiyo itasababisha DUWASA kutozalisha na kusambaza maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Chanzo cha Maji cha Mzakwe kwa siku ya Ijumaa tarehe 19 Juni 2026.
DUWASA inawasihi Wateja wake kuhifadhi maji na kutumia maji kwa uangalifu.
Uzalishaji na Usambazaji wa maji utaendelea mara baada ya TANESCO kukamilisha kazi hiyo kwa kuzingatia ratiba ya mgao wa maji.
DUWASA inaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na
Uhusiano kwa Umma - DUWASA
16.06.2026