News

Posted On: Nov, 05 2021

WAZIRI AZUNGUMZA NA BODI YA DUWASA

News Images

Mhe. Jumaa Aweso (Mb), Waziri wa Maji tarehe 1 Nov. 2021 alifika DUWASA wakati Kikao cha Bodi kikiendelea na kuzungumza na Bodi pamoja na Menejimenti ya DUWASA.

Pamoja na masuala mengine, Mhe. Waziri ameipongeza DUWASA kwa namna inavyofanya kazi nzuri ya kutoa huduma ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zilizopo.

Aidha, Mhe. Waziri ameeleza kuwa Serikali ilitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji ikiwa ni mikakati ya muda mfupi ya kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya maji kwa Jiji la Dodoma.

Vilevile, Mhe. Waziri ameeleza kwamba katika utekelezaji wa mikakati ya muda wa Kati, mradi wa Ujenzi wa bwawa la Farkwa na mradi maji wa Ziwa Victoria itatekelezwa na hadi sasa miradi hii ipo katika hatua mbalimbali ambapo mradi wa bwawa la Farkwa, Serikali inatafuta fedha ili ujenzi uanze. Kwa upande wa Ziwa Victoria, upembuzi na usanifu wa kina utafanyika mwaka huu.

Kuhusiana na mradi mkubwa wa majitaka kwa Jiji la Dodoma, tayari taratibu zipo katika hatua za mwisho ili fedha kutoka Benki ya Exim ya Korea ziweze kupatikana na kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa majitaka.

Mhe. Waziri amewashukuru Wadau wa DUWASA kwa ushirikiano wanaoipatia DUWASA na Serikali kwa ujumla.