News

Posted On: Dec, 11 2024

​WAZIRI AWESO ANADI MIRADI YA MAJI KOREA

News Images

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb) ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya EXIM ya Korea ambayo imefadhili utekelezaji wa miradi ya Majitaka nchini Tanzania yenye jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 248.3 (Mkoa wa Dar es Salaam 90 $US milioni, Dodoma 70 $US million; na Iringa 88.3 $US million).

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisapoti Serikali ya Tanzania kupitia Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utekelezaji wa Miradi ya Maji.

Utelezaji wa miradi hiyo utaimarisha huduma za Usafi wa Mazingira, kuondoa na kutibu majitaka. Vilevile, Tanzania imepata msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8 ambazo zitajenga mfumo wa kusimamia huduma za maji yaani Smart Water Management System (SWMS) katika Mamlaka ya Maji Iringa kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI).