News
WANANCHI NZUGUNI, NDACHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI KAYA ZA KIPATO CHA CHINI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa ushirikiano na shirika la VEI, inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa "Water for Life" wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa majisafi na salama kwa kaya za kipato cha chini katika Kata Mnadani eneo la Ndachi na Kata ya Nzuguni mtaa wa Nzuguni A na B.
Mratibu wa Mradi huo wa Kaya za kipato cha chini, Bi. Mary Godfrey amesema mradi huo unatakiwa kukamilika mwaka huu mwezi Oktoba 2026 kwa awamu ya kwanza ili kupata nafasi ya kuanza kwa awamu ya pili ya mradi.
Ameyasema hayo Augusti 17, 2026 wakati akizungumza na viongozi wa Kata ya Nzuguni ambapo mradi unaendelea kutekelezwa.
Zaidi ya kaya 875 za wanufaika wa mradi wameshafikiwa na wanapata huduma ya majisafi na salama ikiwa ni sawa na asilimia 64 lengo la kufikia kaya 1,250 kwa maeneo ya Nzuguni A, B na Ndachi.