News
Posted On:
Feb, 06 2025
WADAU SEKTA YA MAJI MALAWI WATEMBELEA DUWASA

Februari 05, 2025, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imepokea ugeni kutoka Kampuni ya Usambazaji Maji ya Salima Lilongwe Water Supply Company (SLWSC) ya nchini Malawi kwa lengo la kujifunza namna DUWASA inavyoendesha shughuli zake za uzalishaji na usambazi maji.
Kampuni hiyo ambayo mwenyeji wao ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wametembelea Chanzo cha maji Mzakwe, Kituo cha Kusukuma maji Mailimbili na Tenki la kuhifadhia maji la Mji wa Serikali Mtumba.
Kampuni ya Usambazaji Maji ya SLWSC ya nchini Malawi wameishukuru DUWASA kwa kuwapa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na wameitaka DUWASA kwenda nchini Malawi kujifunza namna wanavyoendesha shughuli hizo nchini Malawi.