News

Posted On: Aug, 18 2022

MWENGE WA UHURU WAFUNGUA MRADI WA MAJI - BAHI

News Images

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndugu Sahili Gereruma amezindua Mradi wa maji katika mji wa Bahi tarehe 16/08/2022.

Mradi huu ulianza kutekelezwa Januari 2022 na kukamilika Juni 2022 ambapo umegharimu shilingi milioni 555 kwa ajili ya kuchimba visima viwili na kulaza bomba kubwa la kutoa maji kwenye visima lenye urefu wa kilomita 2.6 na bomba la Usambazaji lenye urefu wa kilomita 7.5.

Aidha Mradi huu ulikuwa na ujenzi wa tanki kubwa lenye ujazo wa lita 200,000 na vituo viwili vya kuchotea maji.

Sahili amesema vituo vyote vya kuchotea maji (DPs) viwekewe uzio pia amewataka wananchi kuvuta maji majumbani badala ya kuchota kutoka kwenye vituo ili ile dhana ya kutua mama ndoo kichwani iwe na maana.

Kukamilika kwa Mradi huu kunafanya upatikanaji wa maji katika mji wa Bahi kufikia asilimia 94.8 ambapo wakazi 18,000 watanufaika.

Mradi wa Maji katika Mji wa Bahi umefadhiliwa na Serikali kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19