News

Posted On: Nov, 29 2024

​MRADI WA MAJI KISASA - MWANGAZA WAFIKIA 95%

News Images

Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira - DUWASA, Mhandisi Bernard Rugayi amesema Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji Kisasa-Mwangaza umefikia asilimia 95 ya utekelezaji na kwamba baadhi ya wananchi wa maeneo ya Kisasa, Mwangaza na Nyumba 300 Jijini Dodoma wameanza kupata Huduma ya MajI tangu Novemba 21, 2024.

Mhandisi Rugayi amewahakikishia wananchi wa maeneo hayo Novemba 21,2024 wakati akikagua mradi huo, ambapo amesema wananchi watapata huduma ya maji kwa saa 24.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inatekeleza mradi wa kuboresha huduma ya maji eneo la Kisasa ambako kumechimbwa kisima kirefu cha mita 152 chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 1.2 kwa siku.