News
MKUU WA WILAYA YA DODOMA MJINI AKAGUA MIRADI YA MAJISAFI NA MAJITAKA
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Alhaj Jabir Shekimweri amefanya ziara ya kukagua Mradi wa Majisafi wa Nzuguni awamu ya pili na Mradi wa ukarabati na kubadilisha miundombinu wa Majitaka eneo la Area C na D jijini Dodoma leo Julai 9, 2026.
Akizungumza baada ya ziara hiyo Alhaj Shekimweri amesema anaipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na kuwataka kuhakikisha wanamsimamia Mkandarasi ili aweze kuukamilisha mradi wa majisafi wa Nzuguni awamu ya pili kwa haraka zaidi.
Pia amefurahishwa na uwekaji wa vichoteo 18 vya Maji kwa Jeshi la Uokoaji na Zimamoto (Hydrants) kwani ni utaratibu mzuri katika upangaji mji.
Kwa upande wa uboreshaji wa mtandao wa majitaka Alhaji Shekimweli amekemea uchukuaji wa mifuniko ya chemba za majitaka kwani kufanya hivyo ni kuweka mazingira hatarishi kwa watumiaji wa barabara.
Ametoa rai kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa na wenyeviti wa mitaa kusimama kwenye nafasi zao na kuongea na vijana ili kuwabaini wanaofanya uharibifu huo na kuwakamata.