News

Posted On: Dec, 01 2020

MH. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA BWAWA LA FARKWA.

News Images

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ametembelea eneo utakapojengwa mradi wa bwawa la maji Farkwa katika kijiji cha Mombose, wilayani Chemba, mkoani Dodoma, bwawa hilo linatarajiwa kuwa na uwezo wa kutoa maji kwa mita za ujazo 128,000 kwa siku, gharama za ujenzi huo ni zaidi ya sh. bilioni 900.

Aidha, WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maji, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) na Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma wahakikishe mradi huo unaanza mapema.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alitembelea chanzo cha maji cha Mzakwe kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma na kuagiza mkandarasi ambaye anapaswa kuchimba kisima cha kuzalisha maji lita 430,000 kwa saa, aanze haraka kazi hiyo ili kuongeza kiwango cha maji yanayoenda mjini.