News

Posted On: Sep, 16 2026

DUWASA WAKUTANA NA WAWAKILISHI KUTOKA BENKI YA EXIM YA KOREA

News Images

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph pamoja wa wawakilishi toka Wizara ya Maji na Wizara ya Fedha wamekutana na wawakilishi wa Benki ya Exim ya Korea na kujadili kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Mtandao wa Majitaka na Ujenzi wa Mabwawa ya kutibu majitaka katika Jiji la Dodoma.

Majadiliano hayo yalilenga kutatua changamoto mbalimbali zilizopelekea kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa mradi huo. Pia pande zote zilifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ambako mradi unatarajia kutekelezwa ili kujenga uelewa wa pamoja.

Mradi huo unatarajia kugharimu Dola za Kimarekani milioni 70 na utahusisha ujenzi wa mabwawa 16, ukarabati na ulazaji wa mtandao wa mabomba ya majitaka umbali wa kilomita 250.

Kiongozi wa wawakilishi wa Benki ya Exim Korea Ndugu Lee amempongeza Mha. Aron Joseph kwa kuongoza juhudi za ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa mradi huo na amekiri kupitia majadiliano hayo na matembezi waliyofanya wamepata uelewa mpana utakaopelekea kurahisisha maamuzi ya utoaji wa vibali vya utekelezaji wa mradi huo.

Utelezaji wa miradi huo utaimarisha huduma za Usafi wa Mazingira, kuondoa na kutibu Majitaka katika eneo la mradi ndani ya Jiji la Dodoma.