News
Posted On:
Nov, 29 2024
KAYA 1200 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI
Wadau wa kuwezesha miradi ya majisafi kutoka nchini Uholanzi kupitia taasisi ya VEI kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Novemba 26,2024 wamekutana kufanya mapitio na kujadiliana mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Water for Life unaofadhiliwa na VEI katika Kata tatu za Nzuguni, Ndachi na Ntyuka.
Mradi wa kuwaunganishia huduma ya majisafi wananchi 1200 wa Kaya zenye kipato cha chini katika maeneo ya Nzuguni A, Ndachi na Chimala Ntyuka umeanza kutekelezwa mwezi Agosti, 2024 kati ya DUWASA na VEI.
Mradi wa Water for Life unaziwezesha Kaya zenye kipato cha chini kuunganisha huduma ya majisafi kwa gharama nafuu ya shilingi 30,000.