News

Posted On: Feb, 09 2024

KAMATI YA MAJI NA MAZINGIRA YAWASILISHA RIPOTI BUNGENI

News Images

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga leo Februari 09,2024 amesoma Bungeni taarifa ya Kamati hiyo iliyojikita katika masuala ya uanzishwaji wa Gridi ya Maji ya Taifa, uhuishaji wa Sera ya Maji, utunzaji wa vyanzo vya maji, utekelezaji na ukamilishaji wa miradi ya maji kwa wakati na kuanza kutumika kwa mita za maji za malipo kabla.

Taarifa hiyo pamoja na hayo imeelekeza utekelezaji wa kasi wa Mradi wa maji wa miji 28, kutumia Wakandarasi wa ndani katika ujenzi wa miradi, kuboresha mifumo ya majitaka, kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima kwa kutumia magari 25 ya serikali yaliyopo kila mkoa pamoja na kuhakikisha madeni yanakusanywa kwa wadaiwa sugu.

Baadhi ya Wabunge waliochangia katika taarifa hiyo wamesisitiza serikali kutoa fedha za miradi kwa wakati ili ikamilike na huduma iwafikie wananchi kama ilivyokusudiwa