News
Posted On:
Sep, 16 2026
HUDUMA YA MAJI YAREJEA NTYUKA
Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) leo Septemba 16, 2026 wamekamilisha matengenezo ya kisima cha maji kilichopo eneo la Ntyuka Nyerere baada ya hitilafu iliyosababisha wananchi eneo hilo na eneo la karibu kukosa huduma ya maji kwa siku mbili.
Kazi hiyo imefanyika kwa ufanisi ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya majisafi kama ilivyokusudiwa.
DUWASA inawashukuru wananchi wa eneo hilo kwa uvumilivu wao wakati wa kipindi cha matengenezo, na inaahidi kuendelea kuimarisha na kuboresha miundombinu yake ya majisafi ili kuepuka changamoto kama hiyo kujitokeza tena siku zijazo.