News

Posted On: Dec, 05 2024

DUWASA YATEKELEZA MAAGIZO YA AWESO NKUHUNGU

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA)leo Disemba 04, 2024 imekamilisha uchimbaji wa Kisima katika wa Mtaa wa Bochela Kata ya Nkuhungu uliyoanza Disemba 03,2024.

Kisima hicho kimechimbwa katika eneo la Shule ya Sekondari Mnadani ambacho kina urefu wa mita 170 na kinatarajiwa kuwa na maji ya kutosha kuhudumia wakazi wa Bochela na maeneo ya jirani.

Uchimbaji wa Kisima hiki ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb.) na Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde walipotembelea maeneo yenye Changamoto kubwa ya maji ya Nkuhungu na Mkonze jijini Dodoma wakati wa ziara iliyofanyika Oktoba 31,2024.