News

Posted On: Dec, 11 2024

​DUWASA YATANGAZA OFA KWA WATEJA WAKE

News Images

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Lena Mwakisale ametangaza ofa maalumu kwa wateja wake wote waliositishiwa huduma ya maji kulipia nusu ya deni na faini ili kuweza kurudishiwa huduma hiyo.

Bi. Lena Mwakisale ametangaza ofa hiyo Desemba 10, 2024 katika Kituo cha redio cha CFM ikiwa ni ofa ya msimu wa sikukuu za Krismas na mwaka mpya 2025, ambapo wateja wenye madeni zaidi ya shilingi 100,000/- watalipia nusu ya deni pamoja na faini ya 25,000/- ili kuweza kurejeshewa huduma ya maji.

Ofa hii kwa wateja wa DUWASA imeanza tarehe 06/12/2024 hadi tarehe 07/01/2025.