News

Posted On: Mar, 19 2024

DUWASA YASHIRIKI UZINDUZI WA TAARIFA YA UTENDAJI WA MAMLAKA ZA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) leo Machi 18, 2024 imeshiriki uzinduzi wa ripoti ya 15 ya taarifa ya utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka wa fedha 2022/23 uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention.

Ripoti hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na kuzinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri ikiwa ni mwendelezo wa matukio katika kuadhimisha Wiki ya Maji kitaifa jijini Dodoma.

Mhandisi Mwajuma akiongea kwa niaba ya Waziri wa Maji amesema utekelezaji wa watendaji wa Wizara ya Maji kwa kushirikiana na EWURA ndiyo ulioleta mafanikio makubwa katika kufikisha huduma kwa wananchi kufikia lengo la Sera ya Taifa ya upatikanaji maji ya asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mjini

Mhandisi Mwajuma ameeleza kuwa katika kufanikisha utoaji wa huduma bora utekelezaji miradi kwa kutumia vyanzo vya maji vya uhakika umeanza kwa kuwepo na miradi mikubwa ikiwemo mradi wa kutoa maji ziwa Victoria na miradi ya uvunaji wa maji ya mvua

Amezitaka Mamlaka za maji kuweka mkakati wa kuhakikisha zinapambana na kuthibiti upotevu wa maji ambao kwa kiwango kikubwa unachangia ongezeko la gharama za uendeshaji.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema UHAKIKA WA MAJI KWA AMANI NA UTULIVU.