News

Posted On: Jul, 04 2024

DUWASA YASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WILAYA YA DODOMA MJINI

News Images

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira, Mhandisi Bernard Rugayi ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, Leo Julai 3,2024 wameshiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma Mjini ambao umepokelewa katika uwanja wa Shule ya Sekondari John Merlini, Miyuji.

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaj Jabir Shekimweli na utakimbizwa jumla ya KM 45.9 za ndani ya Wilaya ya Dodoma Mjini.

Mbio hizo zinaongozwa na Kauli Mbiu ‘Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa’.