News

Posted On: Aug, 20 2019

DUWASA YASHAURI MATUMIZI MAZURI YA MTANDAO WA MAJITAKA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) imewakumbusha wateja wake na wananchi wote kwa ujumla kutumia vyema mfumo wa mtandao wa majitaka kuepuka mtandao huo kuziba mara kwa mara.

Tahadhari hii inawahusu wananchi wote ambao wameungwa kwenye mfumo wa mtandao wa majitaka na wale ambao hawajaungwa kwenye mfumo wa majitaka pia.

Aidha ikumbukwe kuwa mtandao wa majitaka ni kwa ajili ya taka laini tu na hairuhusiwi kutupa taka ngumu kwenye mfumo wa majitaka.

Inapotokea taka ngumu zikatupwa kwenye mfumo wa mabomba ya majitaka inasababisha kuziba kwa mfumo wa majitaka na kusababisha kero kwa wananchi wengine pamoja na kuweza kusababisha hatari ya magonjwa kutokana na uchafu huo kutapakaa mitaani.

Hivyo, wananchi wote tunahimizwa kujenga chekeche juu ya chemba za majitaka kwa lengo la kuzuia taka ngumu kuingia kwenye mfumo wa majitaka.