News

Posted On: Sep, 09 2026

DUWASA YANUNUA MOTA MPYA 4 KWA AJILI YA UENDELEVU WA HUDUMA YA MAJI DODOMA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imepokea Mota mpya kubwa 4 kutoka kwa Mzabuni ambazo zimegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 430 zenye uwezo wa 250KW kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na uendelevu katika uzalishaji na usambazaji maji kupitia chanzo cha maji cha Mzakwe na kituo cha kusuma maji cha Mailimbili.

Chanzo cha Maji cha Mzakwe ndio chanzo ambacho kinahudumia sehemu kubwa ya Jiji la Dodoma na Mailimbili na ndio Kituo kikuu cha kusambaza maji.

Ununuzi wa Mota hizo unatokana na Motq zilizopo hivi sasa kuanza kuchakaa na hivyo kuhatarisha utoaji wa huduma ya maji endelevu.

Mota hizo ambazo zimepokelewa DUWASA Septemba 08, 2026 ni sehemu ya Mpango wa Serikali wa kusimamia utoaji wa huduma endelevu ya upatikanaji wa Maji katika Jiji la Dodoma.