News
DUWASA YAKAMILISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MITANDAO YA USAMBAZAJI MAJI SAFI.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) imekamilisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa mitandao ya kusambaza majisafi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma.
Akizungumzia kukamilika kwa miradi hiyo Meneja wa Ufundi, DUWASA Mhandisi K. Mayunga amesema, miradi hiyo imekuwa ikitekelezwa katika maeneo mbali mbali kwa lengo la kusogeza huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa Jiji la Dodoma.
“miradi hii imiehusisha kufikisha huduma katika maeneo ambayo yaliyokuwa hayajafikiwa na pia kuongeza ukubwa wa vipenyo vya mabomba kwa maeneo ambayo watu wameongezeka ili kukidhi mahitaji”.
Miradi hiyo imetekelezwa katika maeneo ya Veyula Kambarage, Veyula Muungano, Ndachi Mtube, Ndachi West, Nzuguni A, B na C, Ilazo Extension, Mapinduzi/Makulu, Iyumbu, Nhyuka, Chinangali kaskazini, Chinangali magharibi, Mbwanga na Image.
Aidha Mhandisi aliwasisitiza wakazi wa maeneo husika kufika ofisi kuu ili kufanya taratibu za kuwaunganisha kwenye mfumo wa maji.
“kila mwananchi atakaehitaji huduma ya maji nyumbani kwake ahakikishe kuwa anafika DUWASA na kuonana watumishi husika ambao wanafanya kazi za maunganisho ya maji”.
Kutokana na serikali kuhamia Dodoma na kuongozeka kwa watu na shughuli mbalimbali za maendeleo, maji kama sehemu ya kuwezesha maendeleo hayo, DUWASA imekuwa ikipambana kuhakikisha inakidhi mahitaji ya maji Jijini.