News

Posted On: Mar, 14 2024

DUWASA YAIMARISHA UPATIKANAJI WA MAJI MBANDE - KONGWA

News Images

Hali ya huduma ya maji katika eneo la Kongwa mjini inazidi kuimarika baada ya mabadilko yaliyofanyika kwa kuongeza eneo hilo kuhudumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).

Kazi ya uchimbaji wa visima viwili imekamilika katika eneo la Mbande vyote vikiwa na uwezo wa kuzalisha maji baridi wastani wa lita lelfu 21 kwa saa.

Meneja wa DUWASA wa Kongwa Mhandisi Amran Gama anasema kuwa kazi ya kuweka mtambo wa kuondoa chumvi katika majikatika kisima kingine eneo la Mbande inaendelea na lengo ni huduma ya maji kupatikana kwa saa 24.

Mwenyekiti wa Mbande Peter Chiyumbe anasema huduma ya maji ni nzuri na maboresho yanayoendelea yanatia moyo zaidi. “Sasa tunalipia huduma ya maji kwa namba, hakuna usumbufu” Chiyumbe anasema na kuongeza kulipia huduma sio tatizo na mahitaji kwa wananchi ni makubwa.

Chiyumbe ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo anasema idadi ya wakazi imeongezaeka kutoka enzi za wakazi elfu tatu hadi zaidi ya elfu kumi, hivyo mahitaji nayo yameongezeka zaidi. Anasema kila mwananchi ni mlinzi wa miundombinu kwa sababu maji ndiyo tegemea kuu kwa maisha na kazi za kila siku.

Wizara ya Maji inaendelea na tathmini ya hali ya utoaji huduma kwa wateja wa mamlaka mbalimbali za maji hapa nchini kwa kwa kushirikiana na idara mbalimbali za Serikali na litakuwa endelevu ambapo Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesisitiza mamalaka za maji hapa nchini kuzidi kuimarisha huduma ya maji kwa wananchikwa sababu Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya maji.

Mkurugenzi Msaidizi wa Menejimenti ya Huduma za Maji Mhandisi Lyidia Joseph amesema baada ya miradi kukamilika, sera ya Serikali ni kuhakikisha inatoa huduma bora na toshelevu za maji kwa wananchi.

Ufuatiliaji huu wa huduma za maji umefanyika katika mamlaka tatu za HTM-Korogwe, Bukoba na Dodoma ambapo hali ya maboresho yaliyofanyika ni kubwa kwa maeneo mamlaka hizo waliyoongezewa na matokeo yatafika kwa wananchi.