News
DUWASA YAENDELEA KUFANYA MATENGEZO KINGA KATIKA MITAMBO YA MAJI YA MZAKWE ILI KUKABILIANA MVUA KUBWA ZINAZOTARAJIWA.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeendelea na matengenezo kinga ya mitambo ya kuzalisha na kusambaza maji katika kituo cha Mzakwe, hatua inayolenga kuhakikisha wananchi wanakuwa na huduma endelevu ya maji kutokea chanzo hicho na hawakabiliani na ukosefu wa maji kwa mujibu wa ratiba zao wakati wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Mafundi wa mamlaka hiyo wamekuwa wakifanya kazi ya kuimarisha miundombinu ya maji ikiwemo kituo hicho, kwa kufunga mota mpya na kubadilisha pampu zilizochoka katika baadhi ya visima.
Aidha, DUWASA inawaomba wananchi wote katika eneo lake la huduma, kuchukuwa tahadhali juu ya athari zinazoweza kujitokeza kufuatia mvua kubwa inayotegemewa siku za karibu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa haraka DUWASA kupitia namba za huduma kwa wateja (0800110078 Bure) endapo kuna jambo limetokea na linahitaji kurekebishwa.