News

Posted On: May, 16 2025

DUWASA NA VEI WASAIDIA 'UNIFORM' ZA SHULE KWA SHULE SABA ZA MSINGI KIBAIGWA, KONGWA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kushirikiana na Dutch Water Operators (VEI) wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi 105 wa shule Saba za Msingi zilizopo Kata ya Kibaigwa, Wilayani Kongwa.

Msaada huo wa sare za shule 105 pamoja na vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi wa Shule za Msingi za Sabasaba, Karume, Miembeni, Mzogele, Ndurugumi, Kinangali na Kibaigwa umekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Mayeka Simon Mayeka ambaye alikabidhi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hizo ukiwa na thamani ya shilingi milioni 1.7.

DUWASA na VEI wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maendeleo ya elimu kwa watoto walio kwenye mazingira magumu na wenye uhitaji.

Hafla ya utoaji wa sare na vifaa vya shule kwa wanafunzi imeendeshwa Leo Mei 16,2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Mayeka Simon Mayeka, mgeni rasmi ambaye ameipongeza DUWASA na washirika wake kwa kuonesha moyo wa kujitoa kwa jamii wanayoihudumia.

“Taasisi mbalimbali zinapaswa kujifunza kutoka DUWASA, maana watoto ni wa jamii nzima na jukumu la kulea na kusaidia watoto ni letu sote.” alisisitiza Mhe. Mayeka.

Awali akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bi. Rahel Muhando amesema DUWASA imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji na hiyo imekuwa ni hulka.