News

Posted On: Jun, 17 2026

​DUWASA INASHIRIKI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

News Images

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inashiriki Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma yaliyoanza tarehe 16 Juni, 2026.

Katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, DUWASA inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi, ikiwemo Utatuzi wa changamoto za wateja papo kwa papo, Elimu kwa Umma kuhusu Matumizi sahihi ya Mifumo ya Majitaka, Wajibu wa Mteja kwa Mamlaka na Wajibu wa Mamlaka kwa Mteja.

Aidha, Mteja atapata taarifa za migao ya maji katika maeneo tunayotoa huduma, Elimu kuhusu Bili za maji na mchanganuo wa matumizi na Usomaji wa mita.

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yameanza leo Juni 16, 2026 hadi Juni 23, 2026 ambapo yatamefunguliwa leo Juni 17, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete yakiwa na Kauli Mbiu ya "Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi Kwa Huduma Endelevu"