News
Posted On:
Aug, 27 2024
DUWASA, CCM WAKUTANA
Leo Agosti 27, 2029 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Manzingira Dodoma (DUWASA) wamefanya kikao na Kamati ya Siasa ya CCM Kata ya Nkuhungu jijini Dodoma.
Kikao hicho kilichoongozwa na ndugu Pius Affa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nkuhungu ameiomba DUWASA kutafuta vyanzo vya maji katika eneo hilo ili kuweza kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji Nkuhungu.
Katika kikao hicho baadhi ya wajumbe walitaja baadhi ya maeneo ambayo Mamlaka inaweza kupata vyanzo vingine vya maji na timu ya DUWASA ilifanikiwa kutembelea maeneo hayo ikiwemo eneo la Kanisa la Roma na Kituo cha Afya cha Nkuhungu.