News

Posted On: Jan, 16 2022

BILIONI 7.1 KUPELEKA MAJI YA UHAKIKA ENEO LA VIWANDA NALA.

News Images

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha Intracom kinachojengwa Nala, Jijini Dodoma.

Katika maelezo yake Waziri Mkuu amesema kuwa mahitaji ya maji katika kiwanda hicho ni makubwa ambapo lita 20,000 zinahitajika kwa saa na mpaka sasa upatikanaji wa maji ni lita 7,000 tu kwa saa.

Amesema kuwa Serikali kupitia DUWASA imetenga shilingi bilioni 7.1 kwa ajili kuongeza kiwango cha maji katika eneo hilo la viwanda, kwa kuchimba visima vingine eneo la Zuzu ambako kumegundulika kuwa na maji mengi ya kutosha kuhudumia kiwanda pamoja na wakazi wa eneo la Nala.

Waziri Mkuu amemhakikishia Muwekezaji kuwa maji ya uhakika yatapatikana hivi punde.