News

Posted On: Mar, 24 2021

LIPIA ANKARA YAKO KWA NJIA YA MFUMO WA GePG

News Images

Mfumo wa Malipo ya Serikali wa Kielektoniki (GePG) umeanza kutumika rasmi mwaka 2018, kwa malipo ya serikali na taasisi zake.

Mfumo wa Malipo ya Serikali wa kielektoniki unatumia kumbukumbu namba ambayo mtumiaji (mteja) hupewa katika ankara yake. Namba hii maalum ndio hutumiwa kufanyia malipo ya Serikali au ya Taasisi husika.

DUWASA ikiwa ni moja ya Taasisi za umma chini ya Wizara ya Maji, ilianza kutumia mfumo huu mwezi Machi 2018.

Kurahisisha huduma hii Wizara ya Fedha na Mipango ilianzisha huduma ya kimtandao kwa kutengeneza "application" inayojumuisha taasisi nyingi za umma ikiwemo na DUWASA, Ili kurahisisha upatikanaji wa KUMBUKUMBU NAMBA na kufanya malipo wakati wowote na mahali popote.

Huduma hii nirahisi kutumia, inaokoa muda na gharama kwa tumiaji.

Ili kupata huduma hii fanya yafuatayo:

1. Pakua "App" ya GePG Tanzania katika simu janja yako.

2. Chagua "Water"

3. Chagua DUWASA

4. Ingiza akaunti yako ikianza na A105 au B105

Utapata ankara yako yenye kumbukumbu namba, jina na kiasi unachodaiwa. Pia unaweza kulipa hapo hapo.