TANGAZO

Posted On: Nov 27, 2020


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) inawafahamisha Wateja wake na Wananchi wote kwa ujumla kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Nov. 2020 kuanzia alfajiri ya saa 12 hadi majira ya jioni, DUWASA itazima mitambo ya kuzalisha na kusukuma maji Mzakwe ili kuruhusu matengenezo ya bomba kubwa la inchi 24 eneo la Mbugani Makutupora. Bomba hilo limepasuka na linapoteza maji mengi.

Kufuatia matengenezo hayo, kutakuwa na upungufu wa maji kwa baadhi ya maeneo. DUWASA inawasihi wateja wake kuhifadhi na kuyatumia maji kwa uangalifu ili kuepuka adha ya ukosefu wa maji wakati wa matengenezo. Huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo itarejea katika hali yake ya kawaida muda mfupi baada ya matengenezo wakati kwa maeneo mengine huduma itarejea siku inayofuata kutegemeana na jiografia ya maeneo husika.

Mamlaka inasikitika kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na matengenezo haya.


MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO

Sebastian V. Warioba

DUWASA

26 NOVEMBA 2020