TAARIFA KWA WATEJA WA DUWASA JUU YA MAENDELEO YA MATENGENEZO YA PAMPU KUBWA MBILI ZA VISIMA VYA MAJI AMBAZO ZILIHARIBIKA.

Posted On: Jun 23, 2020


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) inawafahamisha Wateja wake na Wananchi wote wa Jiji la Dodoma kuwa mnamo tarehe 17 Juni 2020 Mamlaka ilifanikiwa kufunga pampu moja kati ya mbili ambazo ziliharibika mwezi Machi 2020 kama taarifa ilivyotelewa na DUWASA.

DUWASA ilichukua hatua ya kuagiza pampu mpya kutoka nje ya nchi lakini kutokana na ugonjwa wa COVID -19unaosababishwa na virusi vya corona, pamp hizo zilichelewa kutengenezwa na kusafirishwa kuja nchini. Baada ya pampu moja kukamilika, DUWASA ilisafirisha kwa Ndege na kuwasili Nchini usiku wa terehe 16 Juni 2020 na kusafirishwa kuja Dodoma tarehe 17 Juni 2020 .

Pampu hizo mbili ambazo ni za visima namba C1 na C3 zilipoharibika mwezi Machi 2020, zilisababisha uzalishaji maji kupungua kutoka wastani wa lita milioni 46 kwa siku na kusababisha baadhi ya maeneo kukabiliwa na upungufu wa maji.

Kazi ya kufunga pampu hiyo ilikamilika majira ya saa sita usiku wa tarehe 21 Juni 2020 baada ya kufanyiwamodifications za kiufundina kuanza uzalishaji maji ambao umeongezeka kutoka wastani wa lita milioni 46 kwa siku hadi kufikia lita milioni 52 kwa siku. Hali ya maji imeanza kuimarika kwenye maeneo mbalimbali.

Pampu nyingine inatarajiwa kuwasili katikati ya mwezi Agosti 2020 na itafungwa mara moja ili kuongeza uzalishaji maji kufikia wastani wa lita milioni 60 kwa siku.

DUWASA inaendelea kufuatilia kwa karibu maeneo yote yenye upungufu wa maji ili kuhakikisha yanapata maji.

DUWASA INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOJITOKEZA KATIKA KIPINDI HIKI.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

DUWASA

23 Juni 2020