TARATIBU ZA MALIPO

Posted On: Jun 12, 2020


Ndugu Mteja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) imepewa jukumu na Serikali la kutoa huduma ya majisafi na uondoshaji wa majitaka kwenye Miji ya Chamwino, Kongwa na Bahi ambapo maeneo hayo yamekuwa ni sehemu ya DUWASA kihuduma. Hivyo, utaratibu wa malipo ya maji utafanyika kupitia mfumo wa Malipo wa Kielektroniki wa Serikali (GePG) kwa njia za mitandao ya Simu, Benki na Wakala wa Benki.

Ili kufanikisha zoezi hili, DUWASA inaomba utupatie namba ya simu ambayo utakuwa unatumiwa ANKARA yako ya maji kila mwezi pamoja na taarifa mbalimbali za huduma ya maji.

TARATIBU ZA MALIPO MBALIMBALI YA HUDUMA ZA DUWASA NI KUPITIA MFUMO WA MALIPO WA KIELEKTRONIKI WA SERIKALI (GePG) KWA NJIA ZA MITANDAO YA SIMU, BENKI, MAWAKALA WA BENKI PAMOJA NA HUDUMA ZINAZOPATIKANA KUPITIA TOVUTI YA DUWASA

 1. JINSI YA KUTAFUTA ANKARA YAKO YA MAJI PAMOJA NA KUMBUKUMBU NAMBA:
 • 1)Piga *152*00# Ok
 • 2)Bonyeza 6 -Maji
 • 3)Bonyeza 1 -DUWASA
 • 4)Bonyeza 1 -Malipo ya maji
 • 5)Bonyeza 1 -Huduma ina makato (Tsh.100)
 • 6)Ingiza akaunti yako ya maji unayotumia kulipa maji mfano 06001609
 1. JINSI YA KULIPA ANKARA YAKO KWA NJIA YA MITANDAO YA SIMU:
 • M-PESA
 • Piga *150*00# Ok
 • Bonyeza 4-Lipa kwa M-Pesa
 • Bonyeza 5-Malipo ya Serikali
 • Kumbukumbu ya namba ya malipo (inayoanza na 9910….)
 • Weka kiasi
 • Weka namba ya Siri – Malipo yataenda kwenye namba 001001
 • Bonyeza 1 Kuthibitisha Malipo
 • TIGO - PESA
 • Piga *150*01# Ok
 • Bonyeza 4-Lipabili
 • Bonyeza 5-Malipo ya Serikali
 • Kumbukumbu ya namba ya malipo (inayoanza na 9910….)
 • Ingiza kiasi
 • Namba ya Siri – Malipo yataenda kwenye namba 001001
 • Bonyeza 1 Kuthibitisha Malipo
 • AIRTEL MONEY
 • Piga *150*60# Ok
 • Bonyeza 5-Lipia bili
 • Bonyeza 5-Malipo ya Serikali
 • Bonyeza 1-Ingiza Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Inayoanza na 9910….)
 • Ingiza Kiasi
 • IngizaNamba ya Siri – Malipo yataenda kwenye namba 001001
 • Bonyeza 1 Kuthibitisha Malipo
 • HALO PESA
 • Piga *150*88# Ok
 • Bonyeza 4-Lipia kwa Halo Pesa
 • Bonyeza 7-Malipo ya Serikali
 • Ingiza Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Inayoanza na 9910….)
 • Weka Kiasi
 • IngizaNamba ya Siri – Malipo yataenda kwenye namba 001001
 • Bonyeza 1 Kuthibitisha Malipo
 • T-PESA
 • Piga *150*71# Ok
 • Chagua 5-Lipia bili
 • Chagua 3-Malipo ya Serikali
 • Ingiza Kumbukumbu namba (Control Number) inayoanzia na 9910…
 • Ingiza Kiasi
 • IngizaNamba ya Siri – Malipo yataenda kwenye namba 001001
 • Bonyeza 1 Kuthibitisha.

MUHIMU:

 • üUnapotakiwa kuweka kumbukumbu namba au kumbukumbu ya malipo weka namba Maalum (Control Number) ya bili, ada au tozo husika.
 • üVilevile unaweza kulipia Benki za CRDB, NMB, NBC na Benki ya Posta.
 • üUnaweza kulipa kwa Mawakala wa Benki popote walipo karibu na wewe.
 1. HUDUMA MBALIMBALI KUPITIA TOVUTI YA DUWASA

Tembelea Tovuti ya DUWASA ambayo ni www.duwasa.go.tz ili upate huduma mbalimbali kuhusu DUWASA ikiwa ni pamoja na taratibu kuhusu:

 • Maunganisho mapya ya majisafi na majitaka.
 • Taarifa mbalimbali na za kila wakati kuhusu DUWASA.
 • Kupata Ankara pamoja na historia ya matumizi na malipo ya mteja.
 • Uondoshaji majitaka.
 • Taarifa mbalimbali za muundo wa DUWASA, majukumu mafanikio,
 • changamoto na mipango ya maendeleo.

MKURUGENZI MTENDAJI

DUWASA